Saturday, June 28, 2014

RUMAFRICA YATENGENEZA POSTER ZA FILAMU YA "INSIDE" YA JENNIFER KYAKA (ODAMA)


Filamu hii Jennifer Kyaka (Odama) ambayo inayonyesha maisha ya wafanyakazi maofisi wanaovyofanya vituko na mabosi wao na wengine hata kumkufuru na kumuudhi Mungu kwa vitendo vya rushwa na uvivu kazini, kwa mana Mungu amesema asiyefanya kazi na asile. Watu badala ya kufanya kazi wanabaki kupiga stori na majungu maofisi. Wadada wanavyotumia uzuri wao kuwalaghai waume za watu kwa kutoa rushwa ya ngono. Hakika kama mcha Mungu ndani ya hii filamu utajifunza mengi na utaburudika na vituko vya wasanii maarufu wa kuchekesha kama KING MAJUTO na  BENY, pia utamuona marehemu RACHEL HAULE, DAVINA, ODAMA, DULLAH WA PLANET BONGO, na wengine wemgi sana. Filamu hii ambayo imetengezwa na kampuni bora Tanzania ya J-FILM 4 LIFE itakuweka mahali fulani KIMAWAZO.Filamu inatoka Julai 10.2014


Tuesday, February 19, 2013

UZINDUZI WA LUGANO MWIGANEGE NI KIBOKO


Lugano Mwiganege ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania siku ya Jumapili aliweza kufanya uzinduzi wa albamu zake mbili ya "UMENIFANYA KUWA NGUZO" na "UMETUKUKA" Uzinduzi huu ulifanyika katika kanisa la Mito ya Baraka lililoko Kariakoo jijini Dar es Salaam. Ashukuriwe Mungu watu wengi walihudhuria katika uzinduzi huo wakiwemo waimbaji maarufu Tanzania kama Masanja Mkandamizaji, Ambwene Mwasongwe, Jackson Betty, Glorious Celebration, Upendo Kilahiro na wengine wengi.

MC wa tamasha hili alikuwa mtangazaji wa Wapo Radio Ritha Chuwalo

Lugano Mwiganege

Mtumishi wa Mungu Lugano Mwiganege aliweza kuimba LIVE nyimbo za kuabudu. Mwimbaji huyu amejikita sana katika uimbaji wa nyimbo za kuabudu. Tamasha hili lilipambwa na vichekesho kutoka kwa Masanja Mkandamizaji pale alipokuwa akihimiza watu kumchangia Bwana Lugano.

Askofu Mwakiborwa alimshukuru Mungu sana kwa hatua aliyofikia Bwana Lugano kwa kufanya kazi ya Mungu anagali ni kijana.

Kulikuwa na waandishi wa habari kutoka Clouds FM ambao walifanya mazungumzo na Bwana Lugano kuhusiana na huduma yake ya uimbaji.

Mwisho mtumishi wa Mungu Bwana Lugano aliwashukuru watu wote waliofika mahali hapo kumuunga mkono kwa kazi yake hii ya uimbaji.

JE WAJUA? Lugano Mwiganege kwa sasa ana blogu yake inayoenda kwa jina la www.mwiganege.blogspot.com ambayo imetegenezwa na RUMAFRICA

Matukio

MC. Ritha Chuwalo wa Wapo Radio
Upendo Kilahiro
 Masanja Mkandamizaji (aliyevalia njano) akiwa na mtoto wa Mtangazaji wa radio wapo Chuwalo
 Jackson Betty kutoka Arusha
 Ambwene Mwasongwe
kutoka kushoto ni silas Mbise wa Wapo radio, Ambwene Mwasongwe, Masanja Mkandamizaji, na huyo mwingine simjui.
 Lugano Mwiganege akiimba moja ya nyimbo zake LIVE
Lugano akitafakari ukuu wa Mungu huku akiwa katika uwepo wa uimbaji.
 Waimbaji waliokuwa kivutio kwa wengi kwa uimbaji wao.
Lugano Mwiganege hakika kazi ya Mungu anaifanya, kama unavyomuona kwa vitendo madhabahuni.

Upendo Kilahiro
 Waliofika kumuunga mkono mtumishi wa Mungu Lugano
Watu wakipokea Baraka za Mungu kwa njia ya nyimbo za kuabudu kutoa kwa Lugano Mwiganege

KADI ZA VIP NI HIZI
Kadi hizi zimetegenezwa na RUMAFRICA wako Sinza Afrikasana sokoni jijin  Dar es Salaam

.Upande wa mbele wa kadi ya mwaliko

Upande wa nyuma wa kadi ya mwaliko

Tuesday, January 29, 2013

LUGANO MWIGANEGE NINAKUKARIBISHA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU YANGU.

Lugano Mwiganege ninayofuraha kukualika Bw, Bi, Mch, Pro, Dr, Miss katika Tamasha la uzinduzi wa albamu ya mbili ya UNIFANYE NGUZO na UMETUKUKA.

Tamasha litafanyika tarehe 17/02/2013 Saa 8:00 - 12:00 jioni. Ukumbi ni katika kanisa la EAGT Mito ya Baraka-Kariakoo (karibu na jengo la Yanga).

Hakutakuwa na KIINGILIO, lakini nafasi ya kushiriki baraka na kuiwezesha huduma hii kuendelea itatolewa.

Wasiliana nasi:
Lugano Mwiganege +255 717 286494 na Deogratius Mariwa +255 758 58628


Lugano Mwiganege.
 Ndani ya Yesu kuna kila kitu..Amini hivyo mtumishi wa Mungu.

BAADHI YA WAIMBAJI WATAKAOKUWEPO KUSHIRIKIANA NA MIMI KUIFANYA KAZI YA MUNGU

 Ambwene Mwasongwe
 Glorious Celebration
 Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji)
 Upendo Kilahiro
Jackson Benty