Tuesday, February 19, 2013

UZINDUZI WA LUGANO MWIGANEGE NI KIBOKO


Lugano Mwiganege ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania siku ya Jumapili aliweza kufanya uzinduzi wa albamu zake mbili ya "UMENIFANYA KUWA NGUZO" na "UMETUKUKA" Uzinduzi huu ulifanyika katika kanisa la Mito ya Baraka lililoko Kariakoo jijini Dar es Salaam. Ashukuriwe Mungu watu wengi walihudhuria katika uzinduzi huo wakiwemo waimbaji maarufu Tanzania kama Masanja Mkandamizaji, Ambwene Mwasongwe, Jackson Betty, Glorious Celebration, Upendo Kilahiro na wengine wengi.

MC wa tamasha hili alikuwa mtangazaji wa Wapo Radio Ritha Chuwalo

Lugano Mwiganege

Mtumishi wa Mungu Lugano Mwiganege aliweza kuimba LIVE nyimbo za kuabudu. Mwimbaji huyu amejikita sana katika uimbaji wa nyimbo za kuabudu. Tamasha hili lilipambwa na vichekesho kutoka kwa Masanja Mkandamizaji pale alipokuwa akihimiza watu kumchangia Bwana Lugano.

Askofu Mwakiborwa alimshukuru Mungu sana kwa hatua aliyofikia Bwana Lugano kwa kufanya kazi ya Mungu anagali ni kijana.

Kulikuwa na waandishi wa habari kutoka Clouds FM ambao walifanya mazungumzo na Bwana Lugano kuhusiana na huduma yake ya uimbaji.

Mwisho mtumishi wa Mungu Bwana Lugano aliwashukuru watu wote waliofika mahali hapo kumuunga mkono kwa kazi yake hii ya uimbaji.

JE WAJUA? Lugano Mwiganege kwa sasa ana blogu yake inayoenda kwa jina la www.mwiganege.blogspot.com ambayo imetegenezwa na RUMAFRICA

Matukio

MC. Ritha Chuwalo wa Wapo Radio
Upendo Kilahiro
 Masanja Mkandamizaji (aliyevalia njano) akiwa na mtoto wa Mtangazaji wa radio wapo Chuwalo
 Jackson Betty kutoka Arusha
 Ambwene Mwasongwe
kutoka kushoto ni silas Mbise wa Wapo radio, Ambwene Mwasongwe, Masanja Mkandamizaji, na huyo mwingine simjui.
 Lugano Mwiganege akiimba moja ya nyimbo zake LIVE
Lugano akitafakari ukuu wa Mungu huku akiwa katika uwepo wa uimbaji.
 Waimbaji waliokuwa kivutio kwa wengi kwa uimbaji wao.
Lugano Mwiganege hakika kazi ya Mungu anaifanya, kama unavyomuona kwa vitendo madhabahuni.

Upendo Kilahiro
 Waliofika kumuunga mkono mtumishi wa Mungu Lugano
Watu wakipokea Baraka za Mungu kwa njia ya nyimbo za kuabudu kutoa kwa Lugano Mwiganege

KADI ZA VIP NI HIZI
Kadi hizi zimetegenezwa na RUMAFRICA wako Sinza Afrikasana sokoni jijin  Dar es Salaam

.Upande wa mbele wa kadi ya mwaliko

Upande wa nyuma wa kadi ya mwaliko

No comments:

Post a Comment